Abdulswammad awapongeza mahafala wa shule ya GreenWood Groove
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir awapongeza mahafala sitini waliofuzu katika shule ya GreenWood Groove Academy huku akiwatakia maisha mema wote walio hitimu katika shule hiyo hususan wale wa shule ya upili tayari kujiunga na vyuo vikuu.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni mwalimu Samuel Nzioki, mfumo huo wa Uingereza yani British National Curriculum ni bora na unamwenzesha mwanafunzi kuweza kujiajiri na kukuza kipaji chake akiwa katika umri mdogo.
Aidha Nzioki amesema mfumo wa 8-4-4 unatofautina sana na mfumo wanao tumia kwani hauna masomo mengi na mwanafunzi husoma kulingana na taaluma yake.
Wakati uo huo amepinga madai kuwa shule kama hizo ni za matajiri pekee na atakaye hitimu katika shule hizo hawezi kujiunga na vyuo vikuu vya humu nchini akisema kuwa mfumo huo umekubaliwa na serikali, na kuna baadhi ya wanafunzi wao walioweza kujiunga na vyuo vikuu humu nchini.
Mmoja wa mahafala walio hitimu katika shule hiyo Stephane Wambui amefurahia kufuzu kwake huku akisema kuwa mfumo huo humwezesha mwanafunzi kufanikiwa maishani kwani hujifunza kulingana na taaluma yake anayo ipenda.
Source: http://radiorahma.co.ke