Wazazi watakiwa kukumbatia mtaala wa Kimataifa kwa elimu bora
Wazazi wamehimizwa kukumbatia mtaala wa kimataifa unaosomeshwa na baadhi ya shule humu nchini, ili kuweza kuboresha viwango vya elimu kwa watoto wao.
Akiongea na wanahabari baada ya sherehe za kufuzu kwa wanafunzi wanaosoma mtaala huo wa IGCSE, katika shule ya Greenwood academy eneo la Nyali mjini Mombasa,Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Samuel Nzioka anasema watoto wengi wanaotoka shule hizo, husomea katika vyuo vikuu bora vya humu nchini na kimataifa na hata kuajiriwa kazi zenye hadhi ya juu.
Aidha amepinga dhana iliyowekwa ya kuwa shule hizo ni zamatajiri pekee na hazilingani na mwendendo wa elimu wa Kenya.
“Kusema kweli kuna dhana ya kwamba iwapo mwanafunzi ameenda kusoma mfumo wa Uingereza hakubaliki hapa Kenya,lazima asomee ng’ambo,hiyo sikweli. Kwasababu kunao wanafunzi wetu ambao wametoka hapa na wanasomea katika chuo kikuu cha Nairobi na vyuo vikuu vyengine hapa nchini kama vile Stathmore,USIU ikionesha kunaowanasomea hapa Kenya. Na pia wanafanya vizuri na kupata kazi nzuri zaidi humu nchini na kimataifa.”Alisema Nzioka.
Nzioki ambaye pia amewahi kufundisha mtaala wa 8-4-4 nchini,ameutaja mtaala huo kuwa kikwazo cha maendeleo kwa wanafunzi wa Kenya kwa mda mrefu,kwani haufundishi kutokana na uwezo wa mwanafunzi bali ni kudidimiza vipaji vya watoto.
Aidha Naibu gavana wa kaunti ya Mombasa, Daktari William Kingi na mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nasiir waliokuwa wageni wa heshima katika warsha hiyo,wamewataka wanafunzi kukumbatia wanayofundishwa huku akiwapongeza waliofuzu katika mitihani yao.
“Kinachohitajika kutoka hapa kwa wale ambao wamefuzu ni kuzingatia yale mliofundishwa na nidhamu mliopata katika shule hii ambayo ni moja wapo ya shule bora nchini,nawatakia kila la kheri katika maisha yenu.” Alisema Abdulswamad.
Kwa upande wa wanafunzi waliohitimu kwenda vyuo vikuu wakiongozwa na Stephen Wambui,wanasema wamejifundisha mengi kutoka shule hiyo na wanaimani kufanikiwa zaidi kimaisha.
Shule ya Greenwood Academy ni mojawapo ya shule bora nchini iliyoko mjini Mombasa inayofundisha mtaala wa kimataifa almaaruf British system.
Source: http://salaamfm.co.ke